Na Mathias Canal, Singida

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwarahisishia huduma za upimaji wa Maralia wananchi wa Kijiji cha Mtamaa.

Tatizo hilo sugu limepatiwa ufumbuzi mara baada ya Mbunge huyo kuwapatia Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 iliyonunuliwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili nchini Kenya.

Mhe Sima amemkabidhi mashine hiyo Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mtamaa Godson Charles Swai mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho ambapo pia ametumia mkutano huo kuwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba Mwaka jana.

Sima alisema kuwa ameamua kuitumia siku hii ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwani wakati wa utawala wake alisisitiza uwajibikaji kwa viongozi kwa kuwatumikia zaidi wananchi kuliko kujilimbikizia mali.

Sima Alisema kuwa Mwalimu Nyerere atakumbukwa zaidi kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwaunganisha watanzania, kutetea usalama wa taifa katika vita vya Kagera dhidi ya Nduli idd Amin, na kufanya uhuru wa kazi na uhuru wa maendeleo.

Alisema kuwa Mwalimu Nyerere katika mambo aliyoyaamini sana na kuyapa mkazo ni pamoja na kupamabana na masuala ya haki usawa kwani alijenga imani katika misingi ya utu,haki na usawa kwa kila Raia wa Tanzania.

Sima ameahidi kuendelea kufanya mikutano mingi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo lake ili kuelezea namna ilani ya uchaguzi inavyotekelezwa kwa vitendo sambamba na kushiriki shughuli za maendendeleo ya wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akimkabidhi mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai kifaa maalumu kwa ajili ya kipimo cha ugonjwa wa Malaria
Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 ikiwa imefunguliwa kwenye Boksi maalumu ili wananchi waione kwa karibu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mtamaa kupitia mkutano wa hadhara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...