Na George Binagi-GB Pazzo
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeanza zoezi la kutembelea maeneo ya ardhi yenye migogoro pamoja na makazi yaliyojengwa kiholela ili kuyafanyia urasimishaji.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, amesema zoezi hilo limelenga kuondoa migogoro yote ya ardhi na kutoa hati ya makazi kwa wananchi ambao makazi yao yaliyojengwa kiholela yatarasimishwa.

Amesema wale waliojenga katika maeneo hatarishi ikiwemo milimani, hawatahusika katika zoezi hilo hivyo wasiendelee na ujenzi wa makazi hayo.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Buhongwa na Luchelele, wameomba migogoro yote ya ardhi inayowakabili ikiwemo kulipwa fidia katika maeneo yao, itatuliwe kwa halmashauri ya Jiji la Mwanza kufanya tathmini upya na katika maeneo yenye migogoro na kutoa hati za umiliki.

Zoezi hili limejili ikiwa siku chache baada ya Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Willium Lukuvi, kufanya ziara Jijini Mwanza na kumtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo kutembelea maeneo yote yenye migogoro na makazi holela kabla ya zoezi za usaminishaji kufanyika.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa jijini humo wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya ardhi yenye migogoro pamoja na makazi yaliyojengwa kiholela kabla ya kuyafanyia urasimishaji na kutoa hati ya makazi kwa wamiliki wake.

Kiomoni alifanya ziara ya kutembelea Kata za Buhongwa na Luchelele na kuzungumza na wakazi wa kata hizo juu ya maeneo yenye migogoro na ambayo bado wananchi wanadai fidia ili kutatua changamoto hizo.
Na BMG
Diwani wa Kata ya Buhongwa, Joseph Kabadi (mwenye suti) akizungumza kwenye ziara hiyo na kuelezea maeneo yenye migogoro ya ardhi katika Kata yake kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi kabla ya urasmishaji wa makazi yaliyojengwa kiholela kufanyika katika kata hiyo. 
Wengine ni viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwemo watendaji wa idara ya ardhi.
Wakazi wa Kata ya Buhongwa Magharibi Kata ya Buhongwa wakiwa kwenye kikao baina yao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kilicholenga kutatua migogoro ya ardhi katika kata hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Luchelele ili kutatua changamoto za migogoro ya ardhi ikiwemo madai ya fidia katika Kata hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...