Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa wa Makazi na Maendeleo Endelevu ya Miji umeanza leo tarehe 17 Oktoba 2016, katika ukumbi wa Casa De La Cultura Ecuatoriana Mjini Quito ,mji mkuu wa Ecuador. 


Mkutano huo wa siku tano unaowakutanisha viongozi wa Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Mashirika ya Kimataifa na wadau mbalimbali umefunguliwa rasmi  na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon. 
Tanzania imewakilishwa na wajumbe saba wakiongozwa na Dkt. Yamungu Kayandabila Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Wengine ni Mhe. Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini, Immaculata Senje Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango miji na Vijiji  kutoka Wizara ya Ardhi, Nehemia Mchechu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Sada Sekiete Afisa Mipangomiji Mkuu kutoka Wizara ya Ardhi, Abdillahi Namwambe Afisa wa Mambo ya Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Fatuma Chillo Mkurugenzi wa Sheria kutoka Shirika la Nyumba la Taifa.
 Ujumbe wa Tanzania  kutoka kushoto ni Dkt. Yamungu Kayandabila Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akiwa mkutanoni hapo pamoja na Mhe. Profesa Anna Tibaijuka Mbunge wa Muleba Kusini na Mama  Immaculata Senje Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango miji na Vijiji  kutoka Wizara ya Ardhi.


Inatarjiwa kuwa matokea ya mkutano huo ni kupatikana kwa  Ajenda Mpya ya tatu  ya Makazi na maendeleo endelevu ya miji,(habitat iii) kwa miaka ishirini ijayo ambayo utekelezaji wake unaenda sawa na utekelezaji wa malengo ya Ajenda 2030 ya Maendeleo endelevu.(SDGs)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...