Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akiongea leo na  umoja wa wamiliki wa Daladala Wilayani Iringa katika ukumbi wa Siasa na kilimo kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabiri.




Na Mathias Canal
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekutana na umoja wa wamiliki wa Daladala Wilayani Iringa katika ukumbi wa Siasa na kilimo kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabiri.
Wakizungumza mbele ya Mkuu wa wilaya hiyo Baadhi ya madereva na Makondakta wameomba kurudishwa katika Stendi ya Miyomboni kama ilivyokuwa hapo awali wakidai kuwa eneo la walilohamishiwa kwa sasa la Mashine tatu ni finyu na lina msongamano mkubwa wa watu jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa wananchi.
Dc Kasesela amesema kuwa kurudi katika standi ya Miyomboni ni jambo lisilowezekana kutokana na eneo hilo kuwa dogo na limezungukwa na makazi ya watu pamoja na majengo makubwa ya biashara jambo ambalo linafanya eneo hilo kuwa hatarishi zaidi kama iwapo kunaweza kutokea janga la moto.
"Unajua Miyomboni ni padogo sana pia pamejibana sasa kama ikitokea moto umewaka pale ni ngumu sana kupafikia kwa wepesi lakini pia Watu wa zima moto ndio waliopendekeza kuwa kituo kile kihamishwe sasa nadhani mnafahamu kuwa sheria ya zimamoto huwa ni ngumu kuipinga", alisema Mhe. Kasesera.
Lakini pia amewataka madereva kuacha kutumika kisiasa kwani wanaofanya hivo wanafanya kwa maslahi yao binafsi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...