THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Upishi duniani aelekea alabama leo

MWAKILISHI kutoka nchini Tanzania katika shindano la Upishi duniani yanayotarajiwa kuanza Novemba 8-15  ameondoka mchana huu kuelekea nchini Alabama kwa ajili ya kwenda kuhakikisha anarudi na ushindi.

Fred Uisso  ni mwakilishi pekee kutoka bara la Afrika kupitia baa ijulikanayo kama Club Afrikando ameweza kuingia katika fainali hizo kwa mara ya kwanza mwaka huu ambapo hatua ya awali iliweza kushirikisha nchi 54 duniani kukiwa na washiriki zaidi ya 3700.

Akiongea kabla ya kuondoka, Uisso amesema kuwa kitu pekee anachoweza kusema kuwa kila analolifanya anamuweka mungu mbele na watanzania wajue kuwa nimeenda kuwakilisha nchi na sio mtu mmoja kwahiyo matumaini makubwa ni dua zao  kuniombea nifanikiwe kurudi na kombe pamoja na kitita cha hela.

Uisso ameweza kuingia katika vinyang'anyiro viwili tofauti, anawania World Stake Championship inayoshirikisha washiriki 50 pamoja na World Chef Championship  ya washiriki 21 ambapo kutakuwa na mashindano ya kupika aina mbalimbali za vyakula ikiwemo vyakula vya asili kutoka nchini kwako.

Kumuweka mungu mbele, kupenda kitu anachokifanya pamoja na nidhamu kimemfanya Uisso kuwa mwakilishi pekee barani Afrika na kutokana na juhudi zake anazozionyesha kampuni ya Red Gold ikaamua kudhamini safari yake ya kuelekea Nchini Alabama.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Red Gold, Darsh Pandit amesema kuwa watanzania wengi hawajui kama kuna mashindano kama haya ila wao kama moja ya kampuni yenye kuhitaji kuona watu wanafanikiwa imeamua kudhamini safari hii na wataendelea kufanya hivyo kila wakati ukitegemea Uisso ni mwakilishi pekee kutoka Afrika na anaenda kupambana na nchi mbalimbali duniani.

Baadhi ya nchi washiriki wa mashindano hayo ni Visiwa vya Haiti, Poturico, Ukraine, Canada, Brazili, wenyeji Alabama na nchi nyinginezo.
Mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Upishi duniani, Chef Fred Uisso akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Masoko Wa kampuni ya Red Gold Darsh Pandit wakati wa safari yake ya kuelekea Alabama, Nchini Marekani.
Mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Upishi duniani, Chef Fred Uisso akipungia mkono wakati wa safari yake ya kuelekea Alabama, Nchini Marekani kushiriki mashindano hayo Duniani.
Mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Upishi duniani, Chef Fred Uisso akiwa katika picha ya pamoja na familia yake.