THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

News Alert: Wafanyabiashara wa DRC warejea bandari ya Dar es salaam

UMOJA wa Wafanyabiashara wa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo (DRC)  Bw. Sumael Edward, ametangaza kurejea kwa wafanyabiashara wa nchi hiyo kutumia Bandari ya Dar es Salaam. 
Bw. Edward alisema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa iadara ya Habari Maelezo.
“Sisi kwa moyo mmoja tumeamua kurejea Bandari ya Dar es Salaam mara baada ya Baba zetu wote wawili Rais John Magufuli na Joseph Kabila kukubaliana mambo mazuri ambayo sisi kama wafanya biashara tunaona yana tija kwetu katika kukuza umoja wetu kati ya Tanzania na DRC”amesema Edward.
 Aliongeza kuwa kwa sasa wanashukuru mizigo yao kwa sasa haikai bandarini kwa kuchelewa na hakuna ubabaishaji wa kupelekwa bandari pasipokuwa na lazima.
 Alimaliza kwa kusema kuwa kwa sasa wananchi wa DR Congo wote wameanza kurejea Tanzania na biashara zote zitakuwa kama zamani na maduka yote Kariakoo yatapata wateja.
Rais wa Wafanyabiashara wa nchini DR Congo Bw. Sumael Edward akiongea na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Tiganya Vicent. 
Picha na Habari na Humphrey Shao wa Globu  ya Jamii


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. HK Anasema:

    Maneno mazuri humtowa nyoka pangoni. Pongezi za dhati kwa Marais wa pande hizo mbili kwa mazungumzo ya pamoja ikiwa ni katika kudumisha na kujenga uhusiano mzuri wa kimaendeleo khususan katika nyanja za kiuchumi na kibiashara mbali ya uhusiano wa karibu sana wa kiujirani na kindugu uliyopo kati ya Tanzania na DRC. Daima umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.