Kwa kutambua umuhimu wa michezo kwa vijana nchini, benki ya NMB imedhamini vijana watano kutoka nchini kwa ajili ya kwenda kushiriki mashindano ya mashua ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Luanda, Angola kuanzia Oktoba 6 - 13, mwaka huu. Akizungumzia udhamini huo wa Milioni 10 na jezi kwa vijana hao.

 Mkurugenzi Mtendaji wa NMB nchini, Ineke Bussemaker amesema NMB kama benki ya kitanzania inawathamini watanzania wote na inajivunia kuwa sehemu ya makampuni ambao yameidhamini timu hiyo ili ikaiwakilishe nchi katika mashindano ya mashua.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB nchini, Ineke Bussemaker akizungumzia udhamini wa NMB kwa timu ya vijana ya mashua ambayo inataraji kushiriki Mashindano ya Afrika ya Mashua.

“NMB ni benki ambayo inaongoza Tanzania na ipo kwa ajili ya watanzania, moja ya sehemu ambayo tunaihudumia ni vijana, tunadhamini michezo mingi na tunaamini ni sehemu nzuri kwa vijana wadogo maana wanatakiwa kuandaliwa mapema,

“Mchezo wa mashua una wachezaji wengi, NMB inajivunia kuwa sehemu ya wadhamini kwa vijana hawa ambao watawakilishi nchi, na tunaamini watarudi kutoka Angola wakiwa na medali,” alisema Ineke.
Nae Makamu Mwenyekiti wa Chama Mashua Tanzania (TSA), Philimon Nassari aliishukuru NMB kwa msaada ambao imewapatia na kuelezea changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiukabili mchezo huo kutokana na kutokuwa na wadhamini wanaowasimamia na kuwaomba NMB kuendeleza udhamini huo kwa kipindi kirefu zaidi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Mashua Tanzania (TSA), Philimon Nassari akiishukuru NMB kwa kuipa timu ya vijana udhamini na kuelezea changamoto ambazo zinawakabili.

“Chama chetu ndiyo kina dhamana ya kuongoza mchezo wa mashua nchini, mchezo huu sio mgeni hata watu wanaovua ngalawa wanatumia mashua, mchezo wetu unadumaa kwasababu hatuna udhamini na kama mnavyojua mchezo huu unachezwa sehemu ya wazi kwahiyo hakuna anayelipa pesa, muda wote niwa kujitolea,

“Mchezo huu kwa sasa nchini unakuwa kama unashuka, tulianza kushiriki na watoto 12 lakini kwa sasa tunakwenda na watoto watano, mwanzo mgumu lakini sisi tunaongeza juhudi na tunawashukuru NMB kwa hili wamelolifanya,” alisema Nassari.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB nchini, Ineke Bussemaker akimkabidhi jezi Kocha wa Timu ya Mashua, Penny Alson.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Dar es Salaam Yacht Club, Robert Cunnane alisema klabu yao imekuwa ikiwasaidia watoto mbalimbali ambao wanacheza mchezo wa mashua kwa kuwapa nafasi ya kujifunza lakini pia muda mwingine kuwalipia fedha kwa ajili ya kwenda kujifunza mchezo huo na matarajio ya klabu hiyo ni kuona mchezo wa mashua unakuwa maarufu nchini.

“Tumekuwa tukisaidia mchezo wa mashua lakini kutoa udhamini kwa kutumia Milioni 24 kila mwaka kwa watoto kwenda kujifunza mchezo wa mashua na kwenda kushiriki mashindano mbalimbali, tunajivunia kuwa na hii timu na tunataka kuona timu hii inapata mafaikio,” alisema Cunnane.
Mwakilishi wa Dar es Salaam Yacht Club, Robert Cunnane akizungumzia jinsi klabu yao inavyoisaidia timu ya mashua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...