Na Dotto Mwaibale
PIKIPIKI
yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi
ya mwaka mmoja katika kituo cha waendesha bodaboda cha Maganga
Veterinary Temeke jijini Dar es Salaam inazua hofu kwa wananchi na hata
kwa askari polisi ambao wameshindwa kuipeleka kituoni.
Imeelezwa
kwamba pikipiki hiyo iliegeshwa katika eneo hilo na mtu mmoja ambaye
alifika nayo akiwa akiiendesha mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza jana na mtandao wa www. habari za jamii.com mmoja
wa waendesha bodaboda wa kituo hicho ambaye hakupenda kujitambulisha
jina lake alisema pikipiki hiyo inawapa hofu wananchi wa eneo hilo na
hata waendesha bodaboda.
"Hata
sisi wenyewe tuna hofu na pikipiki hii ndio maana tunaegesha mbalimbali
na pikipiki zetu na ndio maana sitaki kutaja jina langu" alisema
mwendesha bodaboda huyo.
Aliongeza
kuwa awali baada ya pikipiki hiyo kutelekezwa katika kituo hicho mtu
yeyote alipokuwa akiisogelea au kuigusa ilikuwa ikijiwasha yenyewe
lakini baada ya kupita mwezi mmoja iliacha kujiwasha jambo ambalo
limeongeza hofu kwa wananchi.
Mkazi
mwingine wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Ismail alisema
hata walipotoa taarifa kituo cha polisi cha Maganga walishindwa
kuichukua pikipiki hiyo kutokana na tabia ya kujiwasha.
Alisema
aaskari wa kituo hicho ambacho kipo mita 10 na eneo ambalo ipo pikipiki
hiyo walitoa taarifa kwa wenzao wa kituo cha Chang'ombe ambao nao
wameshindwa kuichukua na kwenda nayo kituoni kwa ajili ya kumtambua
mmiliki wa pikipiki hiyo kupitia namba zake za usajili.
Ismail
alisema inawezekana pikipiki hiyo ilifungwa kifaa maalumu cha utambuzi
iwapo kama imeibiwa na ndio maana ilipokuwa ikiguswa au kusogelewa
inajiwasha yenyewe licha ya baadhi ya watu wanahusisha kujiwasha kwake
na imani za ushirikina.
Imeelezwa
kuwa pikipiki hiyo wakati inatelekezwa ilikuwa katika hali ya upya
lakini hivi sasa imeanza kupoteza upya wake kwa kukosa huduma ya
matunzo.
Jitihada
za mtandao huu kumpata Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo wa Maganga
ili kuzungumzia suala hilo zimeshindika baada ya kuelekezwa alikuwa
Manispaa ya Temeke kwenye mkutano.
Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha bodaboda cha Maganga Veterinary Dar es Salaam.
Mwonekano wa pikipiki hiyo kwa nyuma.
Pikipiki hiyo ikiwa katika kijiwe hicho cha Veterinary Maganga Temeke jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...