THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Polisi Dar yaua wanne waliopora Benki ya CRDB-Mbagala

Na Humphrey Shao,
Globu ya Jamii

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi wanne waliokuwa wamejichimbia katika pori la Mbande jijini Dar es Salaam mara baada ya mapigano makali na majibizano ya risasi yaliyojiri kwa zaidi ya dakika arobaini.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Siro, amesema kuwa jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mmoja wa Majambazi aliyehusika na tukio la ujambazi CRDB Mbagala
"Polisi mara baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na tukio hilo akiwa na wenzie saba hivyo aliwaambia askari kuwa anawapeleka sehemu walipo wenzake kwenye pori la Dondwe ambapo wanafanya mazoezi ya kivita.
"Walipofika katika eneo hilo la mipakani Chanika ghafla majambazi hayo yalianza kufyatua risasi kwenye uelekeo wa askari na mtuhumiwa alikimbia na askari wakaanza kujibu mashambulizi na askari wakafanikiwa kujeruhi majambazi wanne na kufanikiwa kupata bunduki ya kijeshi aina ya SMG iliyofutwa namba za usajili ikiwa na risasi 22 ndani ya Magazine..," amesema Siro.
Amesema kuwa majeruhi hao walikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili na wakati wanapatiwa matibabu wote kwa bahati mbaya walifariki Dunia kutokana na majeraha ya risasi.
Ameongeza kuwa uchunguzi huo umebaini kuwa Bunduki hiyo ni moja ya zile zilizoporwa wakati askari wakibadilishana lindo.