Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wananchi kuwabaini na kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva wote wa malori ya mchanga na kokoto watakaobainika kutofuata sheria za ubebaji wa bidhaa hiyo na hivyo kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara.

Waziri Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma katika ziara yake ya kukagua barabara ya Kidahwe-Kasulu yenye urefu wa kilometa 50 ambapo pamoja na mambo mengine amesema Serikali inatumia fedha nyingi kujenga miundombinu ya barabara kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla hivyo haita mvumilia mtu yeyote atakayebainika kuharibu miundombu hiyo kwa makusudi.

“Kuanzia sasa Serikali haitavumilia madereva wasiozingatia kanuni na sheria za usafirishaji wa mizigo katika barabara nchini, hivyo nawaagiza Mameneja wa TANROADS katika mikoa yote nchini kusimamia sheria ili kudhibiti miundombinu ya barabara, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa ameliomba Jeshi la Polisi kushirikiana vema na makandarasi wanaojenga miundombinu ya barabara katika maeneo mbalimbali nchini kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya watu wasio waaminifu ambao wanaiba vifaa vya makandarasi jambo linalochangia kukwamisha shughuli za ujenzi wa barabara.

Amewataka wananchi wa Wilaya ya Kasulu kutoa ushirikiano kwa mkandarasi wa kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation anayejenga barabara hiyo ili kuwezesha ujenzi huo kukamilika haraka.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya ya Kibondo,alipotembelea ofisi hizo mkoani Kigoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikata moja ya nondo katika ujenzi wa Daraja la Muzye lililopo kwenye barabara ya Kidahwe-Kasulu KM 50 wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akitoka kukagua ujenzi wa daraja la Muzye lililopo kwenye barabara ya Kidahwe- Kasulu KM 50 wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...