THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

PROF. MBARAWA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA

Na Daudi Manongi,MAELEZO

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi teule ya Shirika la Posta kutumia fursa zilizopo ili kuongeza vyanzo vya mapato vya Shirika hilo.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati akizindua Bodi mpya ya wakurugenzi ya Shirika la Posta katika ukumbi wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano leo Jijini Dar es Salaam.

“Nashukuru kwa kuwa mmekubali uteuzi wangu,mmekuja katika shirika zuri na hivyo kama mtajipanga mtaweza kufanya mambo mengi makubwa,naitaji mtu anayeweza kutafta mapato na shirika hili la Posta lina vyanzo vingi lakini bado halijatumika vizuri na hivyo naomba mbadilishe mtazamo wa watu wetu ili msonge mbele” Alisema Prof Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa ameitaka bodi iyo kuisimamia vizuri menejimenti ya Shirika la Posta ili ifanye kazi kwa ufanisi mkubwa na pia amemuagiza mwenyekiti wa bodi hiyo ya wakurugenzi kuwekeana mkakati wa mikataba ya kazi na malengo ili kupata matokeo mazuri na amesisitiza kuboreshwa kwa mahusiano kati ya watendaji wa juu na wafanyakazi wa chini.

Waziri Mbarawa ameagiza bodi iyo teule kusimamia huduma mpya ya Posta mlangoni na Huduma Center kwa uadilifu ili vilete tija kama ilivyokusudiwa na kuihakikishia bodi iyo kuwa serikali imejipanga kulipa Deni la kampuni iyo ili kupunguza mzigo wa utendaji wa shirika hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Luteni kanali Msaafu Haruni Kondo amemhakikishia waziri uyo kuwa wataisimamia vyema menejimenti ya Shirika hilo na kuhakikisha vyanzo vya mapato vinapatikana kama alivyoagiza kwani utekezaji wa majukumu ndio msingi wa maendeleo wa shirika hilo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikata utepe kwenye begi lilobeba vitendea kazi vya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora. 
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. 


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. 


HABARI ZIDI BOFYA HAPA