"Tukio lilianza tarehe Jumatatu 26/9/2016, ambapo Mwalimu Frank Msigwa, mwanafunzi kwa vitendo kutoka Chuo Kikuu cha  Dar Es  salaam ambapo alitoa assignment ya somo la Kiingereza kwa wanafunzi wa kidatu cha tatu.

"Baada ya kusahihisha, aligundua kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hawakufanya. Hivyo, tarehe Jumatano 28/9/2016, alikwenda darasani na kutoa adhabu wale ambao hawajafanya kazi yake. Alianza kwa kuwapa adhabu ya push-up, kisha kupiga magoti na baadae aliwachapa viboko viwili viwli kila mmoja. Katika utekelezaji wa adhabu ile, mwanafunzi  Sebastian Chingulu alikataa kufanya  kutokana na kuumwa na goti.

"Baada ya kuigomea adhabu ile, Mwalimu Frank Msigwa na wenzake wawili, John Deo na Sanke Gwamaka, walimpeleka ofisini na kuanza kumshambulia kwa kipigo kama inavyoonekana kwenye video. Baada ya tukio hilo walimu hao walitoweka shuleni hapo.Wakati wanamshambulia mwanafunzi huyo, kulikuwepo na Mwalimu mwingine aliyewasihi wasiendelee kumpiga kijana huyo na ndiye aliyerekodi tukio hilo.

"Serikali ya mkoa inaendelea kuwashikilia walimu kadhaa pamoja na Mwalimu Mkuu kwa mahojiano pamoja na kupata maelezo ya wanafunzi waliopata adhabu hiyo. Kuhusu mwanafunzi aliyepigwa, nawahakikishia kuwa serikali itawasaka popote walipo walimu  waliofanya tukio hilo na kufikisha katika vyombo vya dola ili wapate haki yao kisheria.
"Aidha mwanafunzi aliyepigwa anaendelea kupimwa na matibatibu.

"Hii ni taarifa ya awali, nitaendelea kutoa 

taarifa kwa kila hatua tunayoifikia..." 

Ni Mimi,Amos G Makalla
Mkuu wa Mkoa wa  Mbeya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sub'hanallah! Pole sana sana Mwanafunzi Sebastian.
    Jamani jamani jamani, hata sisi tumesoma na tumeadhibiwa na pia baadhi yetu tumeipitia hiyo fani na mafunzo hayo hayo kwa vitendo (BTP), lakini ASILAN ABADAN hatujawahi kuadhibiwa wala kuadhibu na hata kupata kuskia au kuona mwanafunzi akiadhibiwa mithli hiyo. Walimu huo tunaodai ni WITO uko wapi hapo? Utadhani mnauwa nyoka jamani ilhali ni binaadam tena mwanafunzi ambae kwa njia moja au nyingine kajaribu kujitetea lakini pia haikusaidia na adhabuye ni almanusura kumdhulumu nafsi yake. Wakati ndio kwanza mlitakiwa mjenge mazingira mazuri na yaliyo rafiki kwa wanafunzi wenu ambayo yatawawia mepesi hata katika zoezi zima la hayo mafunzo yenu kwa vitendo, ambapo hata wakati wa 'assessment' unapofika husaidia na huchangia kwa kiasi fulani the way wanafunzi wanavyo respond darasani, either wakawainua au wakawaangusha katika perfomance zenu, leo mnakwenda kuwa mfano mbaya mithli hiyo, na hiyo 'clip' imeshasambaa ndani na nje ya nch takribani kila mtu kaiona, sana sana ni kuwalaani tu kwa kitendo hicho mlichokionyesha hapo. Kwa kweli inasikitisha na inatilisha huruma na kutia uchungu kwa mlichomfanyia Mwanafunzi Sebastian.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...