KAMPUNI ya EM & U Investiment imeandaa tamasha la Chakula na Vinywaji litakalofanyika (Dar es Salaam Food & Drink Festival) Jumamosi Oktoba 8, 2016  katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Edward James amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake kwa kushirikisha wapikaji  wa vyakula vya asili ikiwa ni kufanya Watanzania kuvipenda vyakula hivyo.
James amesema kuwa watu wengi wanapenda kula vyakula vya asili lakini hawajui watavipata wapi hivyo tamasha hilo litafungua ukurasa mpya juu ya watu kuweza kupata chakula hicho na sehemu gani.
Amesema katika tamasha hilo kutakuwa na wapishi katika kila kabila kupata chakula chake cha asili katika mikoa yao hiyo itakuwa ni sehemu kuwajengea utamdauni wa kupenda chakula cha asili.
James amesema katika tamasha hilo wananchi pia watapata huduma ya kupima afyazao na magonjwa yote bure katika Tamasha hilo wasanii mbalimbali watatumbuza.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ya EM & U Investiment, Bw. Edward James akizungumza na waandishi wahabari juu ya tamasha la vinywaji na vyakula  litakalofanyika viwanja Leaders Club jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mratibu wa Tamasha hilo, Zahara Michuzi  na kulia Meneja Mafunzo na Uwezeshaji, Rashid Chenja.
 Mratibu wa Tamasha hilo Bi. Zahara Michuzi  akielezea juu maandalizi ya  tamasha la vinywaji na vyakula  litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...