THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TAMWA yatoa semina ya uandishi wa habari za usalama barabarani kwa wanahabari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kushoto) akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani leo katika ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (kushoto) akizungumza alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za usalama barabarani leo katika ofisi kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.
Mwasilishaji mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za usalama barabarani yanayofanyika kwa siku tatu kwenye Ofisi Kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.  Mwasilishaji mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za usalama barabarani yanayofanyika kwa siku tatu kwenye Ofisi Kuu ya TAMWA Sinza jijini Dar es Salaam.

MKURUGENZI Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga akizungumza kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo alisema TAMWA ina kila sababu ya kuingia katika mapambano ya ajali nchini kwa kuwa zimekuwa zikiwaathiri wanawake na watoto kwa kiasi kikubwa. 

Alisema licha ya ajali nyingi kupoteza maisha ya wanaume na kujeruhi wengine kundi hilo limekuwa likiwaacha wake zao na watoto pasipo na msaada kwa kuwa wengi humtegemea baba kama mtafutaji katika familia. 

 Alisema wanawake wanaoachwa peke yao na familia wamekuwa wakibeba mzigo mkubwa wa familia jambo ambalo limeendelea kuwaingiza katika hali ngumu. Aidha aliongeza kuwa pamoja na hayo ajali nyingi za waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zimekuwa zikiwaathiri akina dada na akina mama ambao ndio watumiaji wa vyombo hivyo vya usafiri kiasi kikubwa. 

 Tamwa katika mradi huo imejikita katika kutoa elimu ya madereva kuepuka ulevi, ufungaji mikanda ya usalama katika magari, mwendo kasi na matumizi ya kofia ngumu kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria wao. Kwa upande wake Mwasilishaji mada kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu alisema suala la usalama barabarani si jukumu la taasisi moja hivyo kila mtu anapaswa kushiriki katika kupambana na hatimaye kutokomeza ajali hizo ambazo zimekuwa zikipoteza roho za watu, mali pamoja na kusababisha ulemavu kwa baadhi ya waathirika wa ajali hizo.