NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

SHIRIKA la umeme nchini (TANESCO), limekamilisha ujenzi wa  mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) ,  kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo kipya cha kupozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV.

Akizungumzia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa  mfumo huo ambao utahusisha ujenzi wa mfumo wa njia za usambazaji umeme chini ya ardhi (Underground Distribution Lines), wa kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City Centre na vituo vingine vitatu vya Kariakoo, Railway na Sokoine.

Akifafanua zaidi, Mhandisi Rashidi alisema, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmision Lines),  kwa msongo wa Kv132 kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre tayari umekamilika na ule wa kutoka shule ya sekondari ya wasichana Jangwani kwenye City Centre pia umekamilika.
 Kaimu Meneja Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ardhini, (Underground Transmission Lines), kwenye shule ya sekondaru ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2016.

 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashidi wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala,  Mhandisi Athanasius Nangali, (katikati), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashid, (kulia), Afisa Habari na Mawasiliano wa TANESCO, Hendry Kilasila, wakitembelea eneo la ujenzi wa Mfumo huo shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam
 Nguzo ya kusafirisha umeme wa juu kutoka Kituo cha Ilala kuja shule ya sekondari ya wasichana Jangwani, ambapo zitaungana na Mfuko wa njia ya kusafirisha umeme ardhini kupelekea katikati ya jiji

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...