THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

TANZANIA YAWAKILISHWA VYEMA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA MAKAZI NA MAENDELEO ENDELEVU YA MIJI (UN HABITAT III) – QUITO, ECUADORKatibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila akitoa Hotuba katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Makazi na Maendeleo Endelevu ya Miji (UN-HABITAT III, Quito – Ecuador)
Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila baada ya kutoa Hotuba, akipongezwa na Profesa Anna Tibaijuka; Mbunge wa Muleba Kusini, wengine ni Immaculata Senje; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Sada Sekiete- Afisa Mipango Miji Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.  
Katibu Mkuu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila, Immaculata Senje; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Sada Sekiete Afisa Mipango Miji Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika picha ya pamoja na viongozi wa UN-HABITAT Africa Region kutoka Nairobi
Wajumbe kutoka Tanzania, kutoka kushoto ni; Katibu Mkuu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila, Nehemia Mchechu Mkurugenzi Mkuu katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Immaculata Senje; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Fatma chullo Mkurugenzi wa sheria wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakifuatilia Mkutano wa wa Umoja wa Mataifa wa Makazi na Maendeleo Endelevu ya Miji (UN-HABITAT III, Quito – Ecuador)

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano – Wizara ya Ardhi 


Kuna Maoni 3 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Ecuador inatambulika kama nchi ya ulimwengu wa tatu lakini ukifika utashangaa walivyopanga miji yao, barabara ya kisasa, utalii bora. N.K. Yaani bongo hata kupanga mitaa ni shida, saa hizi eti waziri anazunguka na kuhalalisha makazi holela badala ya kusisitiza ujenzi kwa kufuata mpango. Barabara za mitaa humo Quito zote ni paved na clean, n.k. Nadhani nchi kama Tanzania zingejifunza mengi sana kutoka nchi hii. Huwa nashangaa kila mara kwa nini tanzania watu wakijenga nyumba zao hawalazimiki ku-pave eneo la nyumba na kuunganisha na street/barabara ya mtaa. Na kila business au duka lazma liwe na parking lot. Ecuador Ni nchi ya milima na miinuko mingi lakini wamechonga barabara na kuwekeza ktk utalii mpaka utashangaa. Hata ukiingia ktk hospital zao za kawaida utakuta ziko clean na si chakavu kama za Bongo. Sijui mtu ukiwa mweusi inakuwaje kupenda kuendekeza uduni, uchakavu na uchafu!!!!

  2. Mamy Anasema:

    Mimi binafsi ningefurahi kufahamu Mh. Katibu Mkuu amesemea/ujumbe nini kwenye hotuba yake kwenye mkutano huu muhumu wa makazi. Picha sawa

  3. Mamy Anasema:

    Haitoshi kusema Tanzania imewakilishwa vema kwenye mkutano huu. Msemaji wa wizara ambaye na amini yupo na ni sehemu ya ujumbe huu aueleze umma wa watanzania ajenda ya mkutano huu ni nini, mkuu wa wa ujumbe wa tanzania amesema nini katika hotuba yake. Kuweka picha tu na kueleza nani ni nani katika picha kwa maoni yangu bado hujatubarisha kinachojiri kwenye mkutano huu muhimu kuhusu makazi