Timu ya Halotel Tanzania ikipambana na timu ya Mytel wakati wa michuaono ya kombe la dunia la Viettel yanayoendelea katika mji wa Hanoi, nchi Vietnam.
Wachezaji wa timu ya Halotel Tanzania wakisalimiana na wachezaji wa Mytel kabla ya mechi yao kwenye michuaono ya kombe la dunia la Viettel yanayoendelea katika mji wa Hanoi, nchi Vietnam.
Sherehe za ufunguzi za michuano ya Viettel World Cup 2016 nchini Vietnam, ambako timu ya Halotel Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza.



Timu ya Halotel kutoka Tanzania inashiriki katika mashindano ya dunia ya “Viettel World Cup 2016”, yanayofanyika nchini Vietnam katika mji mkuu wa Hanoi yakijumuisha timu 17 kutoka nchi 11 ambazo kampuni ya Viettel imewekeza.

Mashindano hayo yanayohusisha zaidi ya wafanyakazi 10,000 kutoka katika mabara ya Africa, Asia na Latin America huku kilele chake kikitarajiwa kuwa tarehe 15 ya mwezi huu wa kumi.

Toka yalipoanzishwa mwaka 2014, mashindano ya Viettel, yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili, na katika hatua za mwanzo za mashindano hayo yanafanyika kakika nchi zote ambazo Viettel imewekeza.

Dhumuni kubwa la mashindano hayo ni kudumisha ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi wa Viettel na pia kutoa fursa ya kujifunza tamaduni za jamii tofauti tofauti kama njia mojawapo ya kuishi kama familia.

Akiongelea kuhusu mashindano hayo, Mkuu wa Masoko wa Halotel, bwana Ngo duy Truong, amesema mashindano hayo yataimarisha uhusiano miongoni mwa wafanyakazi na pia kuongeza hamasa ya kufanya kazi kama timu moja.

‘Kama kauli mbiu yetu inavyosema ‘Pamoja katika Ubora’ tunaamini kuwa kupitia mashindano haya, wafanyakazi wetu watajifunza umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja na kwa kushirikiana”, akisema bwana Truong.

Mashindano ya kombe la dunia ya Viettel 2016 yanatarajia pia kutoa fursa kwa wafanyakazi wa Viettel kujifunza kuhusiana na tamaduni, historia na geographia ya nchi ya Vietnam.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya Halotel kuingia kwenye mashindano hayo, ambayo yameenda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja wa Halotel toka ilipoanza kutoa huduma zake nchini Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...