HASSAN SILAYO-MAELEZO

Zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma linaloendelea kwa sasa litasaidia kuja na orodha sahihi ya watumishi halali wa umma na kupunguza kabisa idadi ya watumishi hewa serikalini.


akiongea katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari(MAELEZO) kwa ushirikiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Katibu Mkuu Ofisi ya  Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema kuwa zoezi hili limekuwa na mafanikio makubwa kwani  litasaidia kubaini watumishi hewa na kuwatoa katika mfumo wa ajira kutokana na kuiingizia serikali hasara.

“Zoezi hili tunaloliratibu kwa sasa kwa ushirikiano na NIDA litasaidia kuwaondoa watumishi hewa serikalini ambao kwa takwimu imeonesha serikali ilikuwa ikilipa mabilioni ya fedha kwa waajiriwa hewa kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi za watumishi wa serikali jambo ambalo litakoma siku chache zijazo kwa uwepo wa orodha sahihi ya watumishi wa umma” Alisema Dkt. Ndumbaro.

Dkt. Ndumbaro alisema kuwa baada ya kuliendesha kwa mafanikio zoezi hili linatarajiwa kumalizika ndani ya mwezi huu hivyo kuziwezesha taasisi za serikali kuwa na orodha sahihi ya watumishi wa umma hivyo zoezi la kuajiri litaendelea kama kawaida pia kuwaingiza katika mfumo waajiriwa wapya ambao ajira zao zilisitishwa kwa muda.

Aidha Dkt. Ndumbaro alisema kuwa baada ya zoezi hili serikali itajaza nafasi  zote zilizowazi baada ya watumishi hewa kuondolewa katika mfumo wa ajira  serikalini .Wakati Huohuo Dkt. Ndumbaro amesema kuwa upandishaji vyeo kwa watumishi wote wa umma utazingatia utendaji kazi wa mhusika katika eneo lake na kazi.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Suzan Mlay amewataka viongozi wa serikali kutumia lugha nzuri kwa waliochini yao ikiwamo kufuata kanuni sheria na taratibu za kiutumishi katika kutekeleza majukumu yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...