Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe
akipokewa na mkuu wa kitengo cha Kuboresha usalama wa jamii ( DCP)
Godluck Mongi alipokwenda kufungua mafunzo ya upelelezi kwa askari
wa polisi 100. ( katika ni mkuu wa mafunzo wa Jeshi la Polisi DCP Ally
Lugendo. Mafunzo hayo yanafanyika katika chuo cha polisi kidatu
yamefadhiliwa na Tasisi ya Hanns Sidel. Picha na Tamimu adam- Jeshi la
Polisi.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe( katikati)
akiimba wimbo wa maadili wa ofisa wa Polisi wakati wa hafla fupi ya
uzinduzi wa mafunzo ya upelelezi yanayofanyika katika chuo cha polisi
kidatu. Mafunzo hayo kwa askari 100 yamefadhiliwa na Taasisi na Hanns
Sidel.
(picha na Tamimu Adam – Jeshi la Polisi)
(picha na Tamimu Adam – Jeshi la Polisi)
Na. Tamimu Adam - Jeshi la Polisi
Mkuu wa mkoa wa Morogoro mhe. Dkt Kebwe Stevin kabwe amesema Jeshi la
polisi Tanzania ni kioo kwa majeshi ya polisi yalipo Afrika mashariki na hata
afrika kwa ujumla kutokana na umahili wake wa kutoa mafunzo mbalimbali ya
uaskari kwa baadhi ya nchi zilizopo afrika mashariki .
Dkt Kebwe aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya miezi miwili ya
upelelezi katika chuo cha Polisi kidatu yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Hanns Sidel
kwa askari polisi 100 waliotoka katika mkoa wa kipolisi kinondoni ambalo
wamechaguliwa kwa ajili ya kutekeleza kwa weledi mpango wa kuborewsha
usalama wa jamii unaoendelea kutekelezwa katika mkoa huo wa kipolisi.
“Huwezi kwenda kujifunza katika nchi ambayo haifanyi vizuri, na ndioo maana
nchi za jirani huja Tanzania kwa ajili ya kujifunza namna Jeshi la Polisi Tanzania
linavyo weza kuimarisha usalama wa raia na mali zao” alisema Dkt Kebwe.
Aliwataka askari hao wanafunzi wa upelelezi kujifunza kwa makini ili kuboresha
umahiri walionao katika kufanikisha upelelezi ili kuweza kuleta mabadiliko ya
kivitendo katika mkoa wa kinondoni kama eneo la mfano na hatimaye
maboresho hayo yaweze kuenea na kutekelezwa katika mikoa yote nchini hivyo
kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
Kusoma zaidi bofya HAPA.
Kusoma zaidi bofya HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...