Na Emmanuel Matinde-Kigoma

VIJANA wametakiwa kufuata mafundisho ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, juu ya uwajibikaji katika kazi,kuwa wazalendo, kudumisha amani na kuwa walinzi wa amani ya nchi yao.

Mbunge wa Vijana kutoka Mkoa wa Kigoma, Mh.Zainabu Katimba, metoa wito huo juzi katika kijiji cha Katanga wilayani Kakonko, mkoani Kigoma, wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani humo katika siku ya kumbukumbu ya miaka 17 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema wakati wa uhai wake Mwalimu alihubiri uwajibikaji, uzalendo, amani na upendo na kupinga rushwa, hivyo vijana wana wajibu wa kuyazingatia yote hayo kwa manufaa ya taifa.“Tuendelee kufanya kazi ili kumuenzi mwalimu kama vile rais wetu Magufuli anavyofanya kwa vitendo,”alisea Mh.Zainabu.

Kuhusu suala la amani Mh.Zainabu, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Chipukizi Sekondari na vyuo vikuu, alisema vijana hasa waishio mpakani na nchi jirani wanalo jukumu kubwa la usalama wan chi yao kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na kutoa taarifa pindi wanapoona watu wanaowatilia mashaka.

Kauli ya mbunge huyo inakuja siku moja tu baada ya askari polisi wakishirikiana na askari wa jeshi la wananchi kuwaua majambazi wawili waliokuwa wanajiandaa kufanya uhalifu katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko baada ya kukabiliana nao kwa risasi.Nao baadhi ya vijana katika kijiji cha Katanga wakiwemo Nestory John na Honorata Petro, walieleza utayari wao katika kuhakikisha kwamba wanafichua mtu yeyote mwenye nia ya kuhatarisha usalama katika maeneo yao.

Katika ziara yake Mh.Zainabu Katimba, alilenga kukutana na vijana, kusikiliza changamoto zao na kuhamasisha vijana kuanzisha na kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali na yeye kuahidi kushirikiana nao ili kupata fedha za kuanzisha miradi ya ujasiriamali ikiwemo asilimia 5% ya fedha zitolewazo na halmashauri kwa ajili ya vijana.

Vile vile alitoa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya kuwezesha usajili wa vikundi 18 vya vijana katika wilaya za Kigoma vijijini, Buhigwe, Kasulu, Kibondo na Kakonko.
Mbunge wa Vijana kutoka Mkoa wa Kigoma, Mh.Zainabu Katimba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...