THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WACHEZAJI WATATU WA GOLF WA LUGALO WAITWA TIMU YA TAIFA

Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ.

Wachezaji Watatu wa Timu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo wameteuliwa kujiunga na timu ya Taifa ya Mchezo huo ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanzishwa klabu hiyo miaka 10 iliyopita kupata idadi hiyo.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi Jijini Dar es Salaam nahodha wa Klabu hiyo ya Lugalo Kapteni Japhet Masai alisema hatua hiyo ya furaha kwa klabu yao imekuja baada ya mashindano ya wazi ya Arusha Open yaliyomalizika hivi karibuni Jijini Arusha.

”Ni mara ya kwanza na imekuja Muda Mchache baada ya klabu kupata Mwenyekiti mpya Brigedia Jenerali Michael Luwongo pengine ni ishara njema ya Uongozi wake katika klabu hiyo yenye malengo makubwa ya kubor eshwa.” Alisema Masai. 

Aliongeza kuwa Klabu hiyo iliwahi kutoa Mchezaji Mmoka Mwaka 2012 sasa hii ni kwa mara ya kwanza kwa Klabu hiyo kutoa Wachezaji wa Timu ya Taifa zaidi ya mmoja tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo Miaka 10 iliyopita na kutoa mchezaji hata mmoja Tangu Mwaka 2012.

Aliwataja wachezaji hao kutoka Lugalo ni Michael Obare ,Richard Mtweve na Henrick Nyenza ambao wataungana na wachezaji wengine 11 katika mchujo utakaofanyika katika Viwanja vya Klabu ya Lugalo Jumamosi Oktoba 22 ili kupata wachezaji 10 kati yao akiwemo mmoja wa Akiba.

Aliongeza kuwa sasa wachezaji hao wanajiandaa na mchujo ili jumamosi chini ya Uangalizi wa Wachezaji wa kulipwa waweze kufanya vizuri na wajumuishwe katika kikosi huku Wachezaji watalazimika kucheza Mikwaju ya Jumla Gross 74.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa chama cha Golf Tanzania Joseph Tango aliwatangaza wachezaji wengine walioitwa kuwa ni Isack Wanyenche (Kili Golf), Abbas Adam (Moshi Club),Adam Said (Moshi Club).

Wengine walioitwa ni Elisha Mbwambo (TPC),George Sembi(TPC),Victor Joseph (Dar Gymkhana),Amani Said (Dar Gymk(Dar Gymkhana),Salim Shariff (Dar Gymkhana),Idan Iziku (Dar Gymkhana) ,Jay Nathwani (Gymkhana Arusha),Pravin Singh(Gymkhana Arusha). 

Kwa Mujibu wa taarifa hiyo wachezaji hao wanatarajia kuwakilisha Nchi katika mashindano ya Afrika Mashariki East Afrika Golf Challenge Edition 2016 nchini Ethiopia na wanatarajiwa kuanza kambi Jijini Dar es Salaam.

Mchezaji wa Golf wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Michael Obare ambaye ameteuliwa kujiunga na Timu ya taifa akiwa kwenye harakati za Mcheo huo hivi karibuni Jijini Arusha .
Mchezaji wa Golf wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Michael Obare (Wakwanza kulia) ambaye ameteuliwa kujiunga na Timu ya taifa hivi karibuni Jijini Arusha akiwa kwenye mazoezi katika uwanja Lugalo jijini Da es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).