THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Wadau wa habari washindwa kusoma muswada, Kamati yawapa siku 7LICHA ya kupewa zaidi ya mwezi mmoja tangu Bunge lilipoweka hadharani Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari, wadau mbalimbali wa Habari wameshindwa kuwasilisha maoni yao kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii kwa madai ya kutousoma na hivyo kulazimika kupewa siku saba zaidi.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Peter Serukamba alipokuwa akitoa marejesho kwa Waandishi wa Habari mara baada ya kukutana na wadau mbalimbali wa habari nchini kujadili na kupata maoni kutoka kwa wadau hao kuhusu muswada huo.

“Niwapa wadau wiki moja wawe wameleta maoni yao kwa maandishi yaani mpaka Jumatano ya wiki ijayo wawe wameyawasilisha kwa Kamati kwa kuwa leo tumewaita wakasema hawakupata muda wa kusoma,” alisisitiza Mhe. Serukamba.

Mhe. Serukamba ameongeza kuwa mchakato wa kuunda sheria unashirikisha wadau husika kwa kuleta maoni yao juu ya Mswada husika na maoni yao yanasaidia katika kutengeneza sheria iliyo nzuri kwa ajili ya Tasnia ya Habari na maendeleo yake kwa ujumla.

Ameeleza kusikitishwa na wadau hao kushindwa kusoma muswada huo au kuonekana wana ajenda yao na kusisitiza kuwa anaamini kwa muda ambao Kamati imetoa kwa wadau kuwasilisha maoni yao kwa kamati watakuwa wamewasilisha maoni kwa wakati ila kamati iyapitie kabla ya kupelekwa kwa Spika wa Bunge na kuanza kujadiliwa Bungeni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akizungumza wakati wa majadiliano kati ya wadau wa Habari na Kamati hiyo leo Oktoba 19, 2016 Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba(katikati) pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kushoto) na Naibu Sppika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson wakiwasiliza baadhi ya wadau wa habari (hawapo pichani) wakitoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika kikao kilichofanyika leo Oktoba 19,2016 Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel (kushoto) wakiwasiliza baadhi ya wadau wa habari (hawapo pichani) wakitoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika kikao kilichofanyika leo Oktoba 19, 2016 Mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa kamati wakifatilia maoni yaliyokuwa yakitolewa na wadau wa Habari kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika kikao kilichofanyika leo Oktoba 19,2016 Mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa kamati wakifatilia maoni yaliyokuwa yakitolewa na wadau wa Habari kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 katika kikao kilichofanyika leo Oktoba 19,2016 Mjini Dodoma.