Na John Gagarini, Chalinze

KUFUATIA tukio la walimu wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) na cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambao wanadaiwa kumpiga mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Mbeya walimu nchini wameambiwa kupiga wanafunzi siyo njia sahahi ya kufundisha wanafunzi.

Hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete kwenye mahafali ya darasa la saba ya shule ya Msingi Kibiki.

Ridhiwani alisema kuwa baadhi ya walimu wamekuwa wakitumia vibaya ualimu wao kwa kutoa adhabu ambazo haziendani na maadili ya kazi zao.
“Walimu nawaombeni mzingatie maadili ya kazi zenu kwani kuna taratibu za kutoa adhabu na ziko wazi lakini siyo kuwafanyia ukatili wanafunzi kama wale wa Mbeya ambao wameonyesha ukatili wa hali ya juu,” alisema Ridhiwani.

Alisema kuwa mwanafunzi anapaswa kueleweshwa na hata kama ni kupewa adhabu aadhibiwe kwa njia zinazostahili na zinafahamika ambazo si za ukatili na zinazozingatia utu wa mtu.
“Walimu nyie ni walezi hivyo ukiwa mlezi lazima umlee mtoto katika utaratibu kwani endapo unamfanyia ukatili kama huo unamjenga katika mazingira ambayo naye akikua ataona ni hali ya kawaida,” alisema Ridhiwani.

Aliwataka wahitimu hao kutojiingiza kwenye makundi ambayo yanakwenda kinyume cha maadili wakati wakisubiri matokeo ili wasije wakashindwa kusoma vizuri mara waendapo shule za sekondari.

Kwa upande wake mlezi wa shule hiyo Nasar Karama alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa umeme barabara na maji.

Karama alisema kuwa shule inashirikiana na wazazi na walezi katika kukabiliana na changamoto hizo ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri yenye elimu bora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...