THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAWEKEZAJI WILAYANI SERENGETI WAHIMIZWA KULIPA KODI NA KUCHANGIA SHUGHULI ZA MAENDELEO.

Serikali wilayani Serengeti imewataka wawekezaji kulipa kodi na kuchangia katika shughuli za maendeleo ndani ya Wilaya ya Serengeti.

Hayo yamejiri katika katika kikao cha wadau wa maendeleo kilichoitishwa na Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Nurdin Babu alipokuwa akizungumza na wawekezaji waliopo wilayani Serengeti katika ukumbi wa mikutano wa Halmshauri.

“Tunataka kukamilisha ujenzi wa hospitali yetu ya wilaya na nyinyi ni wadau wetu wakubwa katika maendeleo” alisema Mheshimiwa Babu. Aidha Mheshimiwa Babu amesikitishwa na kitendo cha wawekezaji waliopo katika wilaya ya Serengeti kutochangia katika shughuli za maendeleo hali kadhalika kutojitokeza kabisa kwa wahusika wakuu wa makampuni pindi wanapohitajika.

Aidha Mwenyekiti wa Halamshauri ya Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Juma Porini Keya amezitaka kampuni zenye kambi za utalii wilayani Serengeti kulipa kodi na tozo stahiki kwa serikali ili kuiwezesha Serikali kupitia Halmashauri kutoa huduma bora kwa wakazi wa Serengeti. Katika hatua nyingine Mheshimiwa Porini ameziomba kampuni zenye kambi za utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuajiri watu kutoka wilayani Serengeti “Naamini Serengeti wapo vijana wenye sifa za kuajiriwa katika kampuni za utalii hifadhini” alisema Mheshimiwa Porini.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Bw. Juma Hamsini alimpongeza Mkuu wa Wilaya kwa juhudi anazofanya kuhakikisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya unakamilika na kushauri iundwe kamati itakayo wajumuisha wahifadhi pamoja na kampuni za utalii kushughulikia suala la ukamilishaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti.

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ilianzisha mradi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya mjini Mugumu kuanzia mwaka wa bajeti 2007/2008 ili kuimarisha huduma kwa wagonjwa wanaopewa rufaa kutoka vituo 54 vya huduma ya afya vilivyopo wilayani na wale wanaotoka katika mji wa Mugumu na vijiji jirani.

 Aidha wazo la kujenga Hospitali hiyo liliungwa mkono na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuona umuhimu wa ujenzi wa Hospitali hii ili kutoa huduma kwa jamii na wageni wajao nchini kutembelea vivutio vya Kitalii vilivyoko jirani na Mji wa Mugumu hasa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Mpaka sasa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya umekwama kutokana na Halmashauri kutopata fedha kukamilisha ujenzi wa Hospitali.