THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA DAR, KINONDONI KUKAGUA MRADI WA TASAF

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairuki leo amefanya ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAF.

Mh. Kairuki alianza ziara hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa hua Mh. Ally Hapi.
Akiwa ofisini hapo Mh. Kairuki alisaini kitabu cha wageni na kusalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Ally Hapi, wakuu wa wilaya za Ilala, Temeke, Kigamboni na Katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam.

Mara baada ya kusaini kitabu cha wageni, Mh. Angela Kairuki alifanya mkutano na wakuu wa wilaya, wakurugenzi na waratibu wa TASAF Mkoa na manispaa za Dar es salaam ambapo alipokea taarifa mbalimbali za manispaa na Mkoa mradi wa kuondoa umasikini wa TASAF.

Katiba hotuba yake Mh. Kairuki amewataka waratibu wa TASAF wa Mkoa na manispaa kujipanga vema, kusimamia mradi kwa makini na kuondoa wale wote wasiostahili kupata fedha hizo katika orodha ya wanufaika wa TASAF.

Akitoa salam za Mkoa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Ally Hapi amemshukuru Mh. Kairuki kwa ziara hiyo na kumfahamisha kuwa Mkoa wa Dar es salaam unakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa TASAF ikiwemo watu wasiostahili majina yao kuingizwa miongoni mwa wanufaika, kuingizwa kwa majina hewa, kubaguliwa kwa baadhi ya wananchi masikini kwa itikadi za kisiasa na ufuatiliaji duni unaofanywa na waratibu wa TASAF ngazi mbalimbali.

Ziara ya Mh. Angela Kairuki iligusa pia maeneo ya Kata za Kigogo na Msasani ambako Mh. Waziri alipata nafasi ya kuongea na wananchi wanufaika wa TASAF katika mikutano ya hadhara mitaa ya Kigogo Kati na Mikoroshini (Msasani).

Wananchi waliojitokeza wameishukuru serikali kwa mradi huo ambao umekua msaada mkubwa kwao katika kujikwamua na umasikini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairukia akizungumza na mmoja wa wakazi wa Kinondoni,
mara baada ya kufanya ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAFkushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairukia akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,akiendelea na ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAFkushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi