Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii.

Waziri mkuu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Kassim Majaliwa ameiasa Jumuiya  ya Bohora kuja kuwekeza katika nyanja ya viwanda kutokana na Sera nzuri zilizowekwa za uwekezaji na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya jamii ya mabohora Duniani kote na tangu kuanzishwa kwa Taifa hili.

Waziri  Mkuu amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifunga Kongamano la Biashara lililoandaliwa na jumuiya ya Bohora nchini na kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu nyerere, Dar es Salaam.

"Mazingira ya nchi ya Tanzania ni rafiki kwa biashara na uhakika wa soko kutokana na eneo ilililopo kijiografia, kwani nchi yetu inahudumia nchi zaidi ya nane kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam, hivyo kuwa sehemu ya kipekee yenye uhakika wa biashara katika ukanda wa Afrika ya Mashariki" amesema Waziri mkuu Majaliwa.

Amesema kwa sasa serikali yake imejipanga kuziwezsha sekta binafsi zote zinazo hitaji kuwekeza Tanzania hasa katika upande wa Viwanda, hivyo kuwaalika wote ambao wana nia ya kuwekeza kuja hapa nchini na watapata msaada wa kutosha.

Kwa upande wake muwakilishi wa Bohora nchini ,Murtza Adam Jee alimuhakikishia Waziri mkuu kuwa kwa maneno waliyoambiwa na Rais pamoja na yeye sasa viwanda vitakuja, kwani wamejua kuwa hapa ni mahali salama pa kufanya biashara na kujenga Viwanda.

Amesema kuwa kila mfanyabiashara aliyefika hapa nchini amejionea mwenyewe kwa namna gani nchi hii ilivyojiandaa katika uchumi wa viwanda .
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana kiongozi wa Jumuiya ya Bohora Badrul Jamal Bhausaad wakati alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar Es Salaam.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyabiashara wa jumuiya wa Bohora kutoka nchi mbalimbali.
Wafanyabiashara wa Jumiya ya Bohora wakimsikiliza Waziri mkuu katika kongamano la Wafanyabiashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...