Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara katika Mkoa wa Kigoma huku akimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kuunda timu ya uchunguzi juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu tuhuma za wizi wa madawa na ujenzi wa wodi ya kina Mama ya Buhando na ujenzi ulio fanyika Katika zahanati zingine ndani ya Manispaa ya kigoma

Hatua hiyo ya Jafo ilitokana na kutoridhishwa na utendaji wa mkuu wa idara ya Afya ya Manispaa ya Kigoma, John Maganga kutokana na usimamizi mbovu wa miradi hiyo katika idara yake sambamba na kuwepo kwa malalamiko mengi ya ubadhilifu wa madawa ndani ya Manispaa hiyo.

Jafo alitembelea jengo la wazazi la Zahanati ya Buhanda ambapo hakuridhishwa kabisa na maelezo ya ubora wa jengo hilo na mganga mkuu huyo kushindwa kumpa Naibu Waziri maelezo ya kuridhishwa juu ya gharama za ujenzi wa jengo hilo ambalo limejengwa chini ya kiwango na kuwepo mashaka makubwa ya upotevu wa fedha nyingi katika ujenzi wa jengo hilo lililo zinduliwa kinyemela na DMO huyo.

Kutokana na simtofahamu hiyo Naibu Waziri amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kuunda timu ya uchunguzi na kwamba lengo la ziara hiyo ni kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi ndani ya halmashauri mbalimbali hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...