Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Dansi hapa nchini , Ally Choki, anataraji kufanya Tamasha kubwa la kutimiza miaka 30 ya muziki na kuzindua kitabu chake katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni Novemba 26.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Choki amesema kuwa siku ya Onesho hilo watu watapata fursa ya kujinunulia kitabu hicho kinachozungumzia maisha yake yote ya muziki .

"Siku hiyo  tutakuwa na wanamuziki wakongwe wengi kama mzee Zahir Ally Zoro , Hamza Kalala na wengine wengi,ambao ni moja ya watu ninao ingia nao kambini kwa ajili ya shoo hii ya aina yake ambayo inandika historia katika muziki wa Dansi hapa nchini"amesema Ally Choki.

Amemaliza kwa kusema kuwa anawaomba watu watu wajitokeze kwa wingi kwani kingilio ni shilingi 15'000/- kwa kila mmoja .


 Mwanamuziki wa muziki wa Dansi nchini Ally Choki, akionyesha mfano wa kava la kitabu kinachozungumzia maisha yake ya Muziki.
 Mwanamuziki mkongwe Komandoo Hamza Kalala ,akizungumza na waandishi wa habari juu ya maisha ya choki alipokuwa Bantu Group.
 Msemaji wa mwanamuziki,Ally Choki na Mwandishi wa kitabu cha Maisha ya Ally Choki,Juma Kasesa akizungumzia kwa kifupi juu ya kitabu hicho.
Msemaji wa kinywaji cha Windhoek Lager,Andrea Missana akizungumza na wanahabri juu ya kinywaji hicho kudhamini tamasha hilo la miaka 30 ya Ally Choki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...