Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic na Baltic, Mhe. Dora Msechu amepokea picha ya Rais Magufuli kutoka kwa Msanii Mchoraji  Bw. Andrew Dudley Mliga.
 Bw. Mliga amesema kuwa alichukua uamuzi wa kuchora picha hiyo baada ya kuhamasishwa  na kazi kubwa anayofanya  Mhe. Rais ya kuweletea maendeleo Watanzania na ameeleza kuwa yeye ni miongoni wa wanadiaspora wanaopata faraja kubwa kushuhudia jinsi  mafanikio ya uongozi wa Rais Magufuli  yanavyozidi kungarisha  jina la Tanzania kwenye ramani ya Dunia.
Balozi Dora Msechu alipokea picha hiyo kwenye moja ya mikutano ya Jumuiya ya Watanzania Sweden.
Bw. Andrew Mliga ni Msanii Mchoraji  anayeishi Sweden ambaye kazi zake zimejikita zaidi kwenye kuitangaza Tanzania kupitia fani ya uchoraji. Unaweza kujionea baadhi ya kazi zake hapa:   www.safariart.se
 Balozi Dora Msechu akipokea picha ya kuchorwa ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kutoka kwa mchoraji na Msanii Mchoraji Andrew Dudley Mliga.
  Balozi Dora Msechu akipokea picha ya kuchorwa ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kutoka kwa mchoraji na Msanii Mchoraji Andrew Dudley Mliga.
picha ya kuchorwa ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kutoka kwa mchoraji na Msanii Mchoraji Andrew Dudley Mliga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...