Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii.

KUFUATIA kutoa fursa kwa vijana za kujiajiri na kujiendesha kimaisha  benki ya Amana tawi la Mbagala jijini Dar wa Salaam leo limezindua  mkakati wa kuwasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo kwa kutoa mikopo itakayowawezesha kuongeza kipato.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Masoko wa benki hiyo Dassu Mussa amesema kuwa uwezeshaji wa bidhaa hiyo utasaidia ustawi wa biashara ndogondogo kwa kuwawezesha wafanyabiashara kupata mtaji wa kukuza na kustawisha biashara zao.

Mussa amesema kuwa bidhaa hiyo ya uwezeshaji wa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo imeishaanza kutolewa kwa wateja wao wa muda
mrefu kama Raia M.Zubeyya,Ally Nassor na Hussein Bakari ambao walieleza faida ya mikopo hiyo kutoka benki ya Amana.

Moja ya wanufaika wa mkopo huo Raia Zubeyya amesema,"Nashukuru kwa kupata huduma hii, na sijapata usumbufu wowote katika kupata mkopo kwani nimepata huduma nzuri na nimepata mkopo wangu kwa muda muafaka ambao umenisaidia kuendesha biashara yangu"

Mkurugenzi wa benki hiyo Dr.Muhsin Masoud amesema mikopo hii ya wafanyabiashara wadogowadogo ilikuwa ni ndoto ya benki hiyo ambayo waliiweka kwa muda mrefu kwani benki hiyo haikuwa na mikopo tangu kuanzishwa kwake mnamo novemba 2011.

Masoud ameongeza kuwa mikopo hiyo kwa sasa itaanza kutolewa kwenye tawi la mbagala tu lakini kuanzia mwakani matawi yote ya amana Tanzania.

Hata hivyo benki hiyo inawakaribisha wananchi wote Amana benki kwa ajili ya kufungua akaunti na kupata huduma za mikopo kwa ajili ya kuinua biashara na  kukuza biashara zao huku Mgeni mwalikwa  diwani wa kata ya Kibonde Maji Abdalla Mtimika ametoa shukrani kwa uongozi wa benki ya Amana kwa kujumuika nao pia ametoa pongezi kwa kuamua kuanzisha mikopo kwa ajili ya wakazi wake wa Mbagala .
Meneja Masoko wa benki ya Amana, Dassu Mussa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma ya uwezeshaji wa bidhaa ya mkopo kwa wafanyabiashara ndogondogo kwa kuwawezesha kupata mtaji wa kukuza na kustawisha biashara zao.
 Diwani wa kata ya Kibonde Maji Abdalla Mtimika akiwa anatoa shukrani kwa uongozi wa benki ya Amana kwa kuamua kuanzisha mikopo kwa ajili ya wakazi wake wa Mbagala  hususani wafanyabiashara wadogowadogo, kulia ni Mkurugenzi wa benki ya Amana Dr.Muhsin Masoud na kushoto niMeneja Masoko wa benki ya Amana, Dassu Mussa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...