THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yatoa notisi ya siku 30 kwa wadaiwa sugu

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul Razaq Badru akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wadaiwa sugu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari, MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaadizi wa Mawasiliano wa Bodi hiyo Bw. Cosmas Mwaisobwa.

Na: Frank Shija, MAELEZO

Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kupewa notisi ya siku thelethini (30) wawe wameanza kulipa madeni yao kabala hatua zaidi hazijachukuliwa dhidi yao.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul – Razaq Badru alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO kuhusiana na wadai sugu leo Jijini Dar es Salaam.

Badru amesema kuwa notisi hiyo inawalenga wanufaika wa waliokopeshwa na muda wa mataraji ukapita bila wao kuwasilisha taarifa zao na kulipia madaeni ya mikopo ya eleimu ya juu waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/95.

Alisema kuwa jumla ya wanufaika 93,500 walinbainika na kupelekewa Ankara ya madeni yao ili waweze kulipa hata hivyo kati yao ni wadaiwa 81,055 ndiyo wanaendelea kulipa madeni yao.

Aidha Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wapo wadaiwa sugu takribani 142,470 wenye mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 239 hawajajitokeza wala kuanaza kulipa mikopo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dkt. Abdul Mussa amesema kuwa urejeshaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi bilioni 25 zimerejeshwa hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu.

Hatua hii ya kutoa notisi ndani ya siku thelathini inafuatia kutokana na kuvunjwa kwa sheria namba ya 19A (1) cha sheria za Bodi ya Mikopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo pamoja na hatua hiyo Bodi imeazimia kuchukua hatua nyingi za ziada.

Hatua hizo ni pamoja na kuyatangaza majina ya wadaiwa sugu hadharani ili waajiri, wadhamini wao na wadau wengine wenye taarifa za wasugu waziwasilishe,kuwasilisha majina ya wadaiwa kwenye taasisi zinazotunza taarifa za ukopaji na kukamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa hatua za kisheria.