THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Dkt Kalemani azindua mradi wa Umeme (kW 430) mkoani Njombe.

Na Teresia Mhagama.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amezindua mradi wa umeme wa Kilowati 430 unaotokana na maporomoko ya maji katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe ambapo mpaka sasa zaidi ya wateja 1140 wameunganishiwa umeme huku zoezi hilo likiwa ni endelevu.

Uzinduzi huo uliofanyika katika Kata  hiyo ulihudhuriwa na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa wilaya ya Njombe, wananchi wa Kata ya Ikondo, Shirika lililotekeleza mradi huo la CEFA, watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO).

Dkt. Kalemani alisema kuwa mradi huo umetekelezwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya CEFA  kutoka Italia     na kugharamiwa kwa pamoja kati ya Jumuiya ya Ulaya na Serikali ya Tanzania kwa jumla ya Dola za Marekani 110,209.

Aliongeza kuwa mradi huo wa umeme utasambazwa katika vijiji vilivyoko kata za Ikondo, Matembwe na Lupembe na ziada itakayobaki inaingizwa kwenye gridi ya Taifa.

" Habari njema ni kuwa tayari vijiji Saba vimeunganishiwa umeme kupitia mradi huu, hii inatimiza moja ya malengo ya Serikali ya kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa nishati bora katika maeneo ya vijijini kupitia asasi za kiraia," alisema Dkt. Kalemani.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Kilowati 430 katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe.  Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rehema Nchimbi (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Lupembe,  Joram Hongoli (wa pili kushoto),  Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Jane Nunes (wa Tatu kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt Gideon Kaunda (wa pili kulia) na Balozi wa Italia nchini, Roberto Mengoni (wa Nne kulia).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia) akipiga makofi mara baada ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Umeme wa Maji wa Kilowati 430 katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe.  Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rehema Nchimbi (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Lupembe,  Joram Hongoli (wa Tatu kushoto),  Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Jane Nunes (wa Nne kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt Gideon Kaunda (wa pili kushoto). 

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kushoto) akiangalia moja ya mitambo ya kuzalisha umeme  Umeme wa Maji wa Kilowati 430 katika Kata ya Ikondo mkoani Njombe.  Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Rehema na wa kwanza kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga.