THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Kampuni ya Puma Energy Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya ndege 'Vintage Air Rally' za zamani yatakayoanza Novemba 23, 2016


Meneja Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ambamo Mashindano ya Ndege 22 za zamani 'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitatua na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii. Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange,Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mafuta ya ndege,Andrew Lauwo na kushoto ni 

Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari (hawapo pichani) jijini Dar leo, moja ya picha ya ndege 22 za zamani zitakazotua nchini Novemba 28, mwaka huu, kwa mashindano ya 'Vintage Air Rally' yenye lengo la kutangaza utalii. Ndege hizo zilitengenezwa kati ya mwaka 1920 na 1930.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akifafanua moja ya swali lililoulizwa na mmoja Wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, namna ndege hizo za kizamani zitakavyoweza kutumika katika mashindano hayo ya 'Vintage Air Rally' yenye lengo la kutangaza utalii. Ndege hizo zilitengenezwa kati ya mwaka 1920 na 1930.

Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.akijibu maswali ya wanahabari

Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano huo kuhusiana na mashindano hayo adhimu .