JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MALIASILI NA UTALII
TAARIFA
KWA UMMA
MAADHIMISHO KITAIFA YA SIKU YA UTALII DUNIANI NA MAONESHO YA ‘’KARIBU KUSINI’’ 2016
Wizara ya Maliasili na
Utalii kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Mradi wa kuboresha
Mtandao wa Hifadhi za Kusini mwa Tanzania (SPANEST) pamoja na Wadau wa Sekta ya Utalii nchini watashiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii
Duniani kwa mwaka 2016 sambamba na Sherehe
za maadhimisho ya ‘’Karibu Kusini ‘’ Karibu
Tanzania Southern Circuit’’
ambayo Kitaifa yataadhimishwa Mkoani Iringa kwenye viwanja vya Kichangani kuanzia tarehe 25 hadi 29 Novemba, 2016.
Lengo la maadhimisho
hayo ni kuweka uelewa kwa Jamii kuhusu
umuhimu wa utalii na thamani yake ikiwa pamoja na kuutangaza Utalii kwa kuihamasisha jamii
kutumia fursa za utalii zilizopo katika kuinua uchumi wa wakazi wa Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania na Taifa kwa ujumla
Kauli Mbiu ya
maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka
2016 ni “Utalii kwa wote – wote
wawezeshe’’ (Tourism for All – Promoting Universal Accessilibity). Kwa
kuzingatia Kauli Mbiu hii, Serikali inatambua kuwa kuna watu wenye mahitaji maalumu kama vile walemavu, wazee na
watoto ikisisitiza miundombinu rafiki, gharama nafuu kutembelea vivutio vya utalii na gharama nafuu za usafiri
ili
kuhakikisha kwamba, utalii unawahusisha watu wengi zaidi kunufaika nao.
Katika Maadhimisho
hayo, Wizara itakuwa na washiriki ambao ni Idara
pamoja na Taasisi zake mbalimbali. Idara zitakazoshiriki ni
Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki.
Kwa upande wa Taasisi zitakazoshiriki ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha
Taifa cha Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA),
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyamapori (TAWA)
Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS) Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Wadau wa Sekta ya Utalii kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini watashiriki kuonesha
bidhaa na huduma zao muhimu. Mikoa hiyo ni pamoja na Iringa, Njombe, Ruvuma,
Mbeya na Songwe
Aidha, Wizara itatoa punguzo kwa watanzania kutembelea Hifadhi ya Taifa
ya Ruaha pamoja na vivutio vya utalii vilivyokaribu na mji wa Iringa ambavyo ni
Ismila,Kalenga na Boma la Mkuu wa Wilaya kwa gharama nafuu.
Kupitia Maadhimisho hayo wito
unatolewa kwa kuwaalika wadau wote wa utalii na jamii husika kwa pamoja na
kuadhimisha siku hii kama ishara ya jitihada za pamoja za kuufanya utalii nguzo
ya kweli ya maendeleo ya jamii na maendeleo ya jamii ni chanzo cha sekta ya
utalii endelevu zaidi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...