THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Maafisa wa TPA na TRA waanza Mafunzo mara baada ya TPA kukamilisha ufungaji wa ‘Scanner’ mpya Bandari ya Dar es Salaam

 
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akifungua mafunzo hayo kwa Watumishi wa TPA na TRA yanayohusu matumizi ya ‘scanner’ mpya iliyofungwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
 Baadhi ya Watumishi wa TPA ambao watahusika na usimamizi wa matumizi ya ‘scanner’ mpya wakati wa ukaguzi wa mizigo ya kontena katika Bandari ya Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo ambapo aliwasisitiza kuzingatia uzalendo wakati watakapokuwa wanaendesha scanner mpya iliyofungwa katika bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Fredy Liundi, Kaimu Mkurugenzi wa Utumishi, Bw. Erasmo Mbilinyi na Kaimu Mkurugenzi wa Tehama, Bw. Abdulrahman Mbamba (kulia).
 Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deudedit Kakoko akifurahia jambo na Meneja Mafunzo kutoka Kampuni ya Nuctech ya Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Lan Yuming mara baada ya kuzindua mafunzo kwa Maafisa wa TPA na TRA hivi karibuni. Katikati ni Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Nuctech Bw. Zhang Sheng.
Jengo jipya ambalo limejengwa kwa ajili ya matumizi ya scanner mpya iliyofungwa katika bandari ya Dar es Salaam.