THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAKALA YA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI

Na Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog

Hifadhi ya Taifa ya Katavi inapatikana kusini Magharibi mwa Tanzania karibu na Ziwa Tanganyika katika Wilaya za Mpanda ,Tanganyika na Mlele Mkoa wa Katavi inapatikana katika latitude 6.63.7.34 kusini na na longitude 3.74.31.84 Mashariki.

Hifadhi hii ilitangazwa kuwa Hifadhi ya Taifa mwaka 1974 ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 2253 iliongezwa ukubwa mwaka 1996 na kufikia ukubwa wa kilometa za mraba 4471 na kuifanya kuwa Hifadhi ya tatu kwa ukubwa Tanzania baada ya Ruaha na Serengeti .

Ilipata jina lake kutokana na mzimu wa kabila la Wabende aliyejulikana kwa jina la Katabi ambapo mpaka leo watu mbalimbali wamekuwa wakifika ndani ya Hifadhi ya Katavi na kwenda kwenye mti ulioko kwenye Ziwa Katavi wakiamini kuwa mzimu Katabi alikuwa akiishi hapo zamani kabla ya kuwepo Hifadhi ya Taifa ya Katavi .

Jina la Hifadhi hii lilijulikana kama Katabi kutokana na imani ya jamii hizo kwa mzimu Katabi inaaminika kwamba mzimu Katabi una uwezo wa kufanya miujiza ikiwemo kufanya mvua inyeshe , kuzuia magonjwa ya mlipuko kama vile ndui na kutatua shida za watu mbalimbali .
Hawa ni Punda milia wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Kama kibao kinavyo onekana hili ni Eneo la Tambiko ambapo watu huja kusali na kutoa sadaka mbalimbali 
Simba akiwa na mzoga wa Kiboko 
Twiga akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Katavi.