THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAKONDA AWATAKA WAKUU WA WILAYA WOTE KUANZISHA KITENGO MAALUM CHA KISHERIA

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya siku ya  leo ni zamu ya wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni RC Makonda ametoa agizo kwa Wakuu wote wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia agizo lake la kupiga marufuku wenyeviti wote wa Mtaa kutembea na mihuri kwani wamekuwa wanaitumia kinyume na utaratibu kwa kudhulumu haki za wanyonge ikiwemo kuuza viwanja kinyume na utaratibu, huku akisisitiza kuwa watendaji wa mtaa ndiyo inabidi wakae na mihuri hiyo.

Pia RC Makonda amewataka wakuu wa wilaya wote kuanzisha kitengo maalum cha kisheria kitakacho tumika kutoa elimu kuhusu migogoro ya ardhi na kuwashauri wananchi kabla ya kuipeleka mahakamani na kuwaweka wazi kama kuna dalili ya kushinda au vinginevyo na kuwapa suluhisho la kudumu.

Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka DC Hapi na Meya wa Kinondoni Bernard Sita kufuatilia suala la vibali vya ujenzi na kuhakikisha vinatoka kwa wakati ili kuharakisha maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Hapi amehaidi kuwashughukia watendaji wote watakao bainika kutowajibika kikamilifu ili kuchochea maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni ambapo  ametoa agizo kwa Wakuu wote wa wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam kusimamia agizo lake la kupiga marufuku wenyeviti wote wa Mtaa kutembea na mihuri kwani wanaitumia kinyume na utaratibu, leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu  wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi na (kulia) ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
.Mkuu  wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza machache na watumishi wa Manispaa ya Kinondoni leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akipokea ripoti ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda  akiwasili kwenye ukumbi wa Police Officer’s Mess akiambatana na Mkuu  wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi leo jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Manispaa ya Kinondoni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Mi nlikuwa nadhani kamishna wa polisi ni mtu mkubwa saana ila baada ya ziara za makonda naona bora kuwa mwanasiasa kuliko askari wa cheo cha juu.