Ujenzi wa gati la kisasa kuunganisha bandari Kilindoni Mafia na Nyamisati Kibiti unatarajiwa kuanza mwezi Machi mwakani. Hayo yamesemwa mapema leo na Naibu waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Eng Edwin Ngonyani.
Nataka niwahakikishie serikali imetenga bilioni 2.5 kwa kwa ajiri ya ujenzi huu" alisistiza Eng Ngonyani. Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Mafia Mh Mbaraka Dau alionyesha kutoridhishwa kwake na kasi ya utekelezajj mradi huo baada ya meneja wa mradi Agostino Mwenda kusema mchakato utaanza mwisho wa mwezi kwa kufanya utafiti wa udongo baadae taratibu za kumtafuta mkandarasi zitaanza.
" Mheshimiwa Waziri tumemaliza robo mwaka toka kupitisha bajeti, leo meneja anasema wanaanza utafiti wa udongo walikuwa wapi miezi yote minne? Nijuavyo mimi Mheshimiwa Waziri mradi huu unatekelezwa kwa bajeti ya mamlaka ya usimamizi wa bandari TPA kwa kutumia wataalam wake wenyewe iweje leo meneja anasema wanatafuta mkandarasi?" alihoji Mhe Dau kwa mshangao.
Akijitetea meneja wa mradi ndugu Mwenda alikiri kuwepo na mpango huo na kuomba apewe muda ili awasiliane na Mkurugenzi wake mkuu. Naibu waziri aliingilia kati na kuagiza ujenzi ufanywe na mamlaka yenyewe kwa kuwa wana fedha vifaa, na utaalam kutosha.Ziara hiyo ilishirikisha pia Mbunge wa Kibiti Mh Ally Seif Ungando, mwenyekiti wa Halmashauri yao Kibiti Mh Chaurembo, Mkurugenzi mtendaji wa Kibiti, Diwani wa Nyamisati na watendaji waandamizi wilaya ya Kibiti





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...