THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MH. MAJALIWA AMJULIA HALI BABA MZAZI WA WAZIRI MKUU MSTAAFU, MIZENGO PINDA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo kati yake na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda baada ya kuwasili kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma ambako alikwenda kumjulia hali baba mzazi wa Mh. Pinda, Mzee Xavery Kayanza Pinda Novemba 22, 2016. Kulia ni Paroko wa Kanisa Kuu Katoliki la Dodoma , Padri Wisi Onesmo na wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana.
Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa akiongozana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kuelekea wodini wakati alipokwenda kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma kumjulia hali Mzee Xavery Kayanza Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Novemba 22, 2016. Mzee Pnda amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa matibabu.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiteta na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipokwenda kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma kumjulia hali Mzee Xavery Kayanza Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Novemba 22, 2016. Mzee Pinda amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa matibabu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipokwenda kwenye hospitali ya Mkoa wa Dodoma kumjulia hali baba mzazi wa Mh. Pinda, Mzee Xavery Kayanza Pinda Novemba 22, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Wabane sana hao bwana, mimi walinitoa machozi. Unakumbuka?

    Hata, hebu nikumbushe mzee

    WOTE: ha ha ha haaa, iiiii, jamani.