THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Rais wa Zanzibar Dkt. Shein azindua Hospitali ya Abdalla Mzee Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Balozi wa China Nchini Tanzania Mhe. Lu Youqing wakikata utepe kuizindua Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo,iliyojengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Balozi wa China Nchini Tanzania Mhe,Lu Youqing (kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd wakati  akitembelea sehemu mbali mbali za Jengo la Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuizindua rasmi leo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia mashine za kuchunguzia maradhi mbalimbali wakati alipotembelea Chumba cha Maabara katika Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kuizindua rasmi leo akiwa na Balozi wa China Nchini Tanzania Mhe,Lu Youqing (katikati) na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipaa maelezo kutoka kwa Dk.Mariuma Abdalla Salum (kushoto)alipotembelea katika wodi ya wazazi baada ua kuizindua leo,ambayo imejengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd,(katikati) balozi wa China Nchini Tanzania Lu Younqing.
Wananchi waliohudhuria katika uzinduzi wa Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo,ambayo imejengwa na Kampuni ya Kichina Jiang SU Ltd. Picha na Ikulu, Zanzibar.