THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VIJANA SABA WAFUZU MAJARIBIO MAALUMU YA AZAM FC U-17 DAR ES SALAAM

VIJANA saba wenye umri chini ya miaka 17, wamepenya kwenye majaribio ya wazi ya mwisho katika mkoa wa Dar es Salaam, yaliyoendeshwa na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC leo Jumamosi.Huo ni mwendelezo wa mpango wa mabingwa hao wa kutengeneza timu bora ya vijana wa umri huo kwa ajili ya kuwatumia kwa miaka ijayo na wengine kunufaika nao kwa kuwauza.
Katika majaribio hayo walijitokeza vijana 433 wenye umri tofauti kuanzia chini ya umri wa miaka 10, 12, 14 na 17, ambapo waliweza kuchaguliwa saba pekee na wengine 33 kuorodheshwa.
Mpaka sasa mpango huo umeshahusisha mikoa maeneo matano tofauti nchini katika mkoa wa Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma na Visiwani Zanzibar, ambako kote kumefanya idadi ya vijana waliofanyiwa usaili kufikia 2,593, kati ya hao 50 pekee ndio waliochaguliwa kushiriki fainali ya mwisho itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex mwezi ujao.