THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA CCM KUFUATIA KIFO CHA BALOZI MSTAAFU MZEE WAZIRI JUMA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndg. Henry Shekifu kufuatia kifo cha Balozi mstaafu Mhe Waziri Juma (pichani), kilichotokea juzi tarehe 22 Novemba, 2016 jijini Dar es salaam.

Mhe Waziri Juma ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa muda mrefu, Katibu wa CCM ngazi ya Mkoa, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT), pia amekuwa msimamizi wa ujenzi wa reli ya TAZARA, Mkuu wa Mkoa, na Balozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali.
Mhe. Waziri, atakumbukwa na wanachama wa CCM kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi na uimarishaji wa Chama chetu, na kwamba mchango wake katika kupigania na kuleta maendeleo hapa nchini utaendelea kuenziwa na kuthaminiwa na Watanzania.
Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu. 

Imetolewa na:-                    
Christopher Ole Sendeka (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
24.11.2016