THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SENSEI KALONGA: SANAA YA KUJILINDA KWA MIKONO MITUPU (KARATE) NI TAALUMA

Aliyepo katikati ni Rais wa Shirikisho la Karate nchini Tanzania ambaye pia ni mkufunzi wa Goju Ryu Karate Mkoa wa Kilimanjaro Sensei Geofrey Kalonga, wa kwanza kulia ni Sensei Hamis Wembo ambaye ni mkufunzi wa polisi mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Katibu mkuu wa Chama cha Karate mkoa wa Kilimanjaro,aliyepo kulia kwake ni Mkufunzi wa chuo cha polisi Moshi( CCP)Sensei Ibrahim Mganga , wakiwa katika tamasha la kuwatunuku vyeti wanafunzi wa katare waliofuzu mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Mwenge iliyopo Manispaa ya Moshi Mjini.Picha na Vero Ignatus Blog.
Sensei Hamza Mzonge ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa chama cha Karate mkoa wa Kilimanjaro akitoa maelekeza kwa wahitimu mafunzo ya mchezo  wa Karate Mkoa wa kilimanjaro.Picha na Vero Ignatus blog.

Wahitimu wa mafuzo ya karate wakionyesha yale waliyojifinza kabla ya kukabiddiwa vyeti vyao hapo pia wakina dada wamo ndani wakionyesha kata mbalimbali.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mwanadada Matilda Mallya akifanya yake katika karate kwenye tamasha hilo la kukabidhiwa vyeti kwa wahitimu lililofanyika katika ukumbi wa Shule ya Msingi Mwenge iliyopo Manispaa ya Moshi mjini ambapo yeye alipewa cheti kwa kufuzu mafunzo ya mkanda wa brown. Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Karate akipokea cheti chake katika tamasha lililofanyika katika shulke ya msingi Mwenge iliyopo manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.