SERIKALI imeombwa kutengeneza bajeti ya kusaidia taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na kusaidia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ikiwa ndio njia ya kuhakikisha huduma kwa waathirika hao zinaendelea kuimarika.

Imeelezwa kuwa ingawa serikali ndiyo inayotoa dawa za kufubaza makali ya UKIMWI ARVs, haitengenezi bajeti kwa ajili ya wafanyakazi wanaohudumia waathirika kisaikolojia na kitiba.

Hoja hiyo imetolewa na Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA) Jovin Riziki wakati akijibu maswali katika mkutano na ujumbe wa nchi za jumuiya ya NORDIC waliotembelea makao makuu ya PASADA yaliyopo Chang’ombe, Temeke Dare s salaam kuangalia miradi mbalimbali ya kijamii inayofadhiliwa na UNICEF.

Nchi za Jumuiya ya Nordic ni wafadhili wakubwa wa miradi inayoendeshwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA) Jovin Riziki (kushoto) akitoa maelezo kwa sehemu ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) katika chumba cha kuhifadhia kumbukumbu za wagonjwa ulipotembelea kwenye kituo hicho cha PASADA jijini Dar es Salaam. Kulia ni kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders Rönquist.(Habari picha na Zainul Mzige )

Akijibu swali nini ambacho atataka kumweleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikutana naye, Riziki alisema kwamba angelipenda kuona serikali inawajibika kusaidia huduma katika taasisi mbalimbali zinazoigusa jamii zinaendelea kutolewa.

Alisema asasi zinazosaidia waathirika wa UKIMWI kama hiyo ya PASADA hutegemea asilimia 100 misaada ya nchi na wafadhili wa kigeni ambapo miradi ikimalizika mara nyingi waliokuwa wanahudumiwa hukosa mahali pa kupata misaada iliyokuwa inawawezesha kuendelea kuishi kiutu kwa kuwa na siha njema na kufanya shughuli za kiuchumi.
Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA), Jovin Riziki (kushoto) na ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa mtoa huduma katika kitengo cha dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKIMWI ARV's ulipotembelea kwenye kituo hicho cha PASADA jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...