THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SIKU YA TAIFA YA TAKWIMU AFRIKA YAADHIMISHWA LEO JIJINI DAR

Na Amina Kibwana- Globu ya Jamii. 

Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali leo wameadhimisha siku ya takwimu afrika kwa lengo la kuongeza uelewa mpana kwa watumiaji wote wa takwimu Afrika na kuhusu umuhimu wa Takwimu katika kupanga mipango ya maendeleo katika sekta zote za kijamii na kiuchumi.

Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr.Albina Chuwa amesema kuwa faida za kuwa na takwimu za kiuchumi katika mtengamano wa kikanda na miundo yake kwa Nchi yetu ni wa muhimu sana hususan kwa wakati huu ambao serikari yetu inapigania uchumi wa viwanda, Hivyo uboreshaji wa takwimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ni jukumu shirikishi likiongozwa na Ofisi ya Takwimu.

Chuwa amesema kuwa kwa kutumia kauli mbiu hii "Kuimarisha Takwimu za kiuchumi kwa Mtangamano wa Kikanda, Mabadiliko ya Miundo na Maendeleo Endelevu", ambayo ilitolewa na Umoja wa jumuia ya Afrika kwa kushirikiana na Ofisi ya takwimu Afrika itasaidia kuimarisha na kuboresha umuhimu wa takwimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya Mgeni rasmi Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na watoto,Dr.Khamisi Kigwangalla kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inaenda sambamba na Utekelezaji wa Malengo endelevu ya Maendeleo ya Dunia ya mwaka 20130,Agenda ya Afrika ya mwaka 2063 na mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2016 na 2017 hadi 2020 na 2021 kwa lengo la kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa Duniani, bara la Afrika na  Tanzania kwa ujumla.

Dkt. Kingwagalla amesema kuwa umuhimu wa Takwimu za Uchumi haziwezi kukwepeka, akaongeza kusema kuwa ni lazima Watakwimu na wachumi wote ndani na nje ya Afrika na hususan hapa Nchini ambapo wana jukumu la kuhakikisha wanatimiza wajibu wao waliotumwa na wananchi kwa kuleta maendeleo ya kweli ndani ya Serikali ya Awamu ya tano yenye kauli mbiu ya Hapa kazi tu.

"Kuwepo kwa takwimu za kiuchumi zenye ubora kunasaidia sana katika kupanga mipango bora ya kiuchumi na maendeleo ya jamii, hivyo basi tunahitaji kuona takwimu za kiuchumi zinapatikana kwa wakati na zenye ubora unaofuata kanuni zilizowekwa na ofisi ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa na kwa kutumia ubora wa uhakika".

Siku ya takwimu Afrika imeanzishwa na Bodi ya Umoja wa Mataifa, Kamisheni ya uchumi ya Afrika ( UNECA), Wachumi na watakwimu tangu mwaka 1990, ambapo siku hii pia hutoa fursa kwa Nchi kutathmini na kufuatilia malengo yaliyofikiwa katika Mipango ya Maendeleo ya ndani ya nje ya nchi.