THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


SIMU.TV: Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amelishutumu jeshi la polisi kuwa linatumiwa kuvuruga mikutano ya chama hicho. https://youtu.be/OGUtM-bNd1Y

SIMU.TV: Wananchi wa kijiji cha Likuyu senga Maganga mkoani Ruvuma wamechangishana nauli kwa ajili ya kutuma wajumbe kwenda kwa waziri wa ardhi kufikisha malalamiko yao ya kunyang’anywa ardhi. https://youtu.be/WmwPK90LImo

SIMU.TV: Uhaba wa mafundi wa vifaa tiba katika hospitali za rufaa na za kanda umeelezwa kuwa changamoto inayokwamisha wagonjwa kupatiwa matibabu kwa wakati. https://youtu.be/cDfcvbDUC14

SIMU.TV: Sakata la ubadhirifu wa miradi ya maendeleo jijini Dar es Salaam limeendelea kuwatikisa wenyeviti wa mitaa baada ya kuibuliwa kwa kero mbalimbali kwenye ziara ya mkuu wa mkoa huo. https://youtu.be/YtPv93XqL5U

SIMU.TV: Ukosefu wa mabeni na usafiri kwa wananfunzi wa chuo cha Ufundi stadi Veta mkoani Lindi umeelezwa kuwa changamoto inayokwamisha vijana wengi kupata mafunzo ya ufundi stadi. https://youtu.be/Ln9uJ772z0I

SIMU.TV: Serikali ya mkoa wa Shinyanga umewaagiza wakulima kulima zaidi zao la pamba baada ya kupatikana kwa soko la uhakika kwenye kiwanda cha nyuzi. https://youtu.be/MTC6GrqMK8I

SIMU.TV: Akina mama wa mji wa Mankaka wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara wameshindwa kujitokeza kushiriki zoezi la kufanya usafi kutokana na kuhangaikia huduma ya maji. https://youtu.be/OaBlZ9JgKpc

SIMU.TV: Wadau wa michezo nchini wameiomba serikali kutengeneza miundombinu ya mchezo wa viatu vyenye matairi ili kuweza kuinua mchezo huo. https://youtu.be/nRT8yq3zIBs

SIMU.TV: Serikali imewataka vijana kutopuuza michezo mbalimbali kwa maana ni njia ya kujijengea afya bora na ajira pia. https://youtu.be/tXnFJdpapCY

SIMU.TV: Kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake Sebastian Mkoma ameeleza kuwa timu hiyo itanufaika na ligi ya wanawake kwa kupata wachezaji wazuri zaidi. https://youtu.be/V8D0X63hbNo

SIMU.TV: Wachambuzi wa mpira wa miguu kutoka sehemu mbalimbali duniani wamesifu juhudi za kocha wa klabu ya Chelsea kwa kufanikiwa kuibadilisha timu hiyo kwa muda mfupi. https://youtu.be/9rNJqoLXAIM