KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imefunga huduma za mawasiliano ya
intaneti bure katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
itakayowawezesha madaktari, wafanyakazi wengine, wagonjwa pamoja na
wananchi wanaofika katika kituo hicho kupata huduma ya mawasiliano ya
intaneti bure yenye kasi ya hali ya juu.
Akikabidhi
huduma hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba alisema kampuni hiyo imetumia jumla ya
shilingi milioni 120 kufunga huduma bure ya intaneti katika kituo hicho
na itatolewa kwa muda wa mwaka mmoja ikiwa ni kuiwezesha taasisi hiyo
kuendesha shughuli zake kwa ufanisi.
Akifafanua
zaidi Bw. Kindamba alisema huduma hiyo ambayo itagharimu shilingi
milioni 10 kwa kila mwezi ambazo zitakuwa zikilipwa na TTCL ikiwa ni
mchango wake kwa jamii na hasa kwa matibabu yanayofanyika katika kituo
hicho itakuwa ikitolewa kwa teknolojia ya Wi-Fi bure kwa kipindi cha
mwaka mmoja kuanzia Novemba 10, 2016 hadi Novemba 10, 2017.
"Kwa
kuzingatia umuhimu wa sekta ya afya na kazi kubwa inayofanywa na
Taasisi hii, TTCL tumetoa intaneti yenye kasi hadi kufikia spidi ya
100Mbps, spidi hii itasaidia kuongeza uwajibikaji katika kutoa huduma
kwa wananchi, kuimarisha mawasiliano miongoni watumishi wa JKCI na nje
ya Taasisi, kupashana habari za kitabibu na kubadilishana taarifa za
kitabibu miongoni mwa wataalamu kutoka hospitali za ndani na hospital za
nje ya mipaka ya Tanzania," alisema Kindamba.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo. Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL kukabidhi huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi akifuatilia.
Picha ya pamoja mara baada ya zoezi la makabiadhiano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...