THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

UPDATES: MWILI WA MAREHEMU SPIKA MSTAAFU WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMUEL SITTA KUWASILI KESHO TAREHE 10 NOVEMBA ,2016

Mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu wa Mhe. Samuel Sitta unatarajiwa kuwasili kesho Alhamisi Novemba 10, 2016 majira ya saa 9:00 alasiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mwili huo unatarajiwa kupokelewa na Viongozi Mbalimbali wa Kitaifa wa Chama na Serikali katika eneo la Terminal I.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo Jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Waziri Mkuu, mara baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege, mwili huo utapelekwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es saam.

Aidha, taratibu za viongozi mbalimbali na wanaombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mhe.Sitta zitafanyika katika Viwanja vya Karimjee siku ya Ijumaa ya tarehe 11 Novemba ,2016 kuanzia majira ya saa 1:30 asubuhi.

Mara baada ya zoezi hilo kukamilika mwili wa Marehemu Sitta utapelekwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea mkoani Dodoma siku ya Ijumaa tarehe 11 Novemba, 2016.

Mwili huo utawasili mkoani Dodoma majira ya saa 8 mchana na kupokelewa na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma na Bunge.

Baadae mwili huo utapelekwa katika Viwanja vya Bunge ambapo salamu mbalimbali zitatolewa na Spika, Waziri Mkuu , Kambi Rasmi ya Upinzani na viongozi wa Mkoa wa Dodoma.

Mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, Waheshimiwa Wabunge na waombelezaji mbalimbali walioko katika Viwanja vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma watatoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu na baadaye kupelekwa Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa ajili ya kusafirishwa kwenda Urambo mkoani Tabora kwa ajili ya mazishi.

Mwili wa Marehemu Sitta unatarajiwa kuwasili Uwanja wa Ndege wa Tabora majira ya saa 10 jioni ya 11 Novemba, 2016 na baadae kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Wilayani Urambo ambapo utawasili majira ya saa 12 jioni.

Viongozi na waombezaji mbalimbali Wilayani Urambo mkoani Tabora watatoa heshima za mwisho siku ya Jumamosi tarehe 12 Novemba, 2016 kuanzia asubuhi na mazishi yanatarajia kufanyika siku hiyo hiyo majira saa 9 alasiri.

Marehemu Mhe. Sitta alizaliwa 18 Desemba, 1942 Urambo Mkoani Tabora

Imetolewa na Idara ya Habari- Maelezo
9 Novemba, 2016