THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

VIWANDA VINAJENGWA KWA KASI MKOA WA PWANI-MWIJAGE

Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji, Charle’s Mwijage  amefanya ziara kutembelea viwanda vilivyopo Mkoa wa Pwani na kuangalia maendeleo ya mkoa huo katika sekta ya viwanda.Katika ziara hiyo Waziri Mwijage alipotembelea kiwanda cha Viuadudu cha kibaha, Sayona Fruits, Global Packaging kiwanda cha kuunganisha matrekta pamoja na kiwanda cha Eveline.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara hiyo, Mwijage  amesema ujenzi wa viwanda katika mkoa wa Pwani unakua kwa kasi na kuonngeza ajira kwa watanzania.

Amesema kitendo cha mmiliki  wa kiwanda cha Sayona kuwapa  wanakikjiji  fursa ya kupata elimu mpaka ngazi ya chuo kikuu na kisha kuajiliwa katika kiwanda hicho ni uungwana ambao watafanya kazi ya kufundisha wafanyakazi wenzao.

“Wafanyakazi wa Sayona kupatiwa fursa ya kwenda chuo kikuu kujifunza ili kuja kuwafundisha wenzao, kasi hiyo imenifurahisha sana” amesema Waziri Mwijage.
 Waziri  wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kuwasili mkoani pwani kwaajili ya ziara ya siku moja.
 .Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s akizungumza na meneimenti ya kiwanda cha viua vidudu kilichopo kibaha, mkoani Pwani Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwada hicho,Samwel Mziray mkoani Pwani. 

 Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akipata maelezo kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda Viua Vidudu hicho,Samwel Mziray katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama. 
 Waziri  wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha viua vidudu, Kibaha.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA