THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WASOMI WATAKIWA KUWA WABUNIFU KATIKA KUPATA AJIRA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

IMELEZWA Kuwa bado kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa ajira kwa wahitimu wa mafunzo ya elimu ya juu licha ya kuwepo kwa vyuo vya kutosha nchini.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa mafunzo ya ufundi na Amali wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Mwajuma Pembe alipokuwa akifunga kongamano la siku mbili la wasomi na wakufunzi wa vyuo vikuu nchini jijini Dar es Salaam.

“Bado kuna changamoto kubwa sana licha ya kuwepo kwa wahitimu wa elimu ya juu kila mwaka hali inayotokana na upungufu wa viwanda hapa nchini hivyo ndio maana serikali ya awamu ya tano inasisitiza uchumi wa viwanda hili kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira hapa nchini”amesema Waziri Pembe.

Waziri huyo ametoa wito kwa wasomi na wahitimu wote hapa nchini kuwa wabunifu katika kila jambo wanalosomea hili kuweza kujikwamua kiuchumi na kutumia elimu waliyonayo katika mazingira yanayowazunguka.

Alimaliza kwa kusema kuwa wanazuoni wanatakiwa kuja na majibu muafaka ambayo yatawezesha wahitimu kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kujiajiri katika masuala mbalimbali.
 Waziri wa Elimu na  mafunzo ya amali wa serikali ya Mapindzu Zanzibar, Mwajuma Pembe akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu wakisikiliza kwa makini wakati wa kufunga kongamano hilo

 Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar , Mwajuma Pembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo.


 . Mjumbe wa kamati ya maandalizi  wa mkutano huo, Thea Mtau, akimkaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar , Mwajuma Pembe.